Wazazi shuleni St. Monica walalamikia matokeo duni na kuongezewa karo

  • | Citizen TV
    178 views

    Asilimia kubwa ya wazazi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya St. Monica wameandamana mjini kitale hadi ofisi za Mkurugenzi Tume ya Huduma za Walimu, TSC na ile ya Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu wakishinikiza mwalimu mkuu wa shule hiyo kuhamishwa huku wakikataa kuwarejesha wanafunzi wao shuleni waliotumwa nyumbani baada ya kushiriki maandamano wiki moja iliyopita.. Baadhi ya sababu zilizowachochea kuandamana ni pamoja na matokeo duni, na kuongezewa karo isiyo halali. Wazazi hao wamepokelewa na kamishna wa Kaunti hiyo, Gideon Oyagi ambaye amesema tayari maafisa wa Idara ya Upelelezi, DCI wanaendeleza uchunguzi na kutoa amri kwa wasimamizi wa elimu kaunti hiyo kuhakikisha kwamba hatua mwafaka zinachukuliwa ili masomo yasitatisike wakati huu ambapo wanafunzi wanajiandaa kwa mtihani wa kitaifa.