Waziri Kindiki akanusha madai kuwa wanafunzi 70 kutoka shule ya Hillside wamepotea

  • | K24 Video
    28 views

    Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki, amekanusha vikali madai kuwa wanafunzi 70 kutoka shule ya bweni ya Hillside Endarasha wamepotea kufuatia moto mkubwa ulioharibu bweni la wavulana alhamisi iliyopita. Tukio hilo, ambalo limeiacha nchi ikiomboleza, lilisababisha vifo vya wavulana 21, huku serikali ikiahidi kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha haki inatendeka.