Waziri Murkomen asema polisi wa akiba katika Bonde la Kerio watakaguliwa upya

  • | Citizen TV
    1,663 views

    Maafisa wote wa Polisi wa akiba wanaohudumu katika Bonde la Kerio linalokumbwa na utovu wa usalama watafanyiwa upya ukaguzi kabla ya kurejea kazini. Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen, ametoa agizo hili wakati wa mkutano wa usalama Elgeyo Marakwet ambapo alifichua kuwa baadhi ya maafisa hawa wamekuwa wakishirikiana na wahalifu. Ben Kirui anaarifu kutoka kaunti hiyo ya Elgeyo-Marakwet.