Wiki ya kimataifa ya watoto wa mitaani yaadhimishwa Kisii

  • | Citizen TV
    151 views

    Washikadau mbalimbali kutoka kaunti ya Kisii walikongamana katika uga wa Gusii kusherehekea wiki ya kimataifa ya watoto wa kurandaranda mitaani. Katika hafla hiyo ,Mamia ya vijana wa kurandaranda mjini Kisii walitumia fursa hiyo kuzungumzia masaibu yao mitaani wakitaka serikali na mashirika yasiyo ya serikali kuwakumbuka na kuwasaidia kupata huduma za matibabu na masomo. Aidha maafisa kutoka mashirika mbalimbali walitoa wito wa ushirikiano ili kuwasaidia vijana hao wengine walio na talanta maalum ili kutimiza ndoto zao maishani.