Wito watolewa kwa walimu kukumbatia teknolojia katika mfumo wa sasa wa masomo ili wasibaki nyuma.

  • | K24 Video
    20 views

    Ulimwengu leo unasherehekea siku ya walimu huku wito ukitolewa kwao teknolojia katika mfumo wa sasa wa masomo ili wasibaki nyuma. Katika kaunti ya Machakos walimu bora wametuzwa kutokana na bidii yao ya kuleta mabadiliko katika masomo hasa katika maeneo yanayoonekana kuwa kame nchini. Walimu mia moja na kumi wametuzwa na shirika lisilo la kiserikali la kenya connect kwa kuimarisha uchu wa wanafunzi wa masomo ya teknolojia na uboreshaji wa mazingira wanayosomea. Tume ya kuajiri walimu, TSC Imekiri kwamba matumizi ya teknolojia katika mfumo wake umeimarisha utoaji wa huduma kwa walimu.