Wizara ya utalii na wanyamapori yaanzisha mpango wa kulipa fidia kupitia mfumo wa dijitali

  • | K24 Video
    19 views

    Wizara ya utalii na wanyamapori imeanzisha mpango wa kulipa fidia kupitia mfumo wa dijitali ili kuharaskisha malipo kwa familia zilizoathiriwa na mizozo kati ya binadamu na wanyamapori kote nchini. waziri rebecca miano, ametangaza kuwa kamati maalum imeundwa kusimamia mchakato huo na kushughulikia changamoto chini ya sheria ya uhifadhi na usimamizi wa wanyamapori ya 2013. serikali tayari imetenga shilingi bilioni 15 ili kutekeleza mradi huo.