Yuko wapi Jonathan Nabwera?

  • | Citizen TV
    2,005 views

    Kwa majuma mawili sasa, familia ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta Jonathan Nabwera Simiyu imekuwa ikimtafuta baada ya kwenda kwa hafla ya sherehe na rafikize. Jonathan mwenye miaka kumi na tisa hajaonekana tangu tarehe 28 alipokuwa eneo la utawala. Familia yake sasa ikitaka msaada wa serikali kumtafuta kijana huyu ambaye hata simu yake imekuwa mteja asiyepatikana.