Yuko wapi Omar Abdulrahman?

  • | Citizen TV
    2,385 views

    Familia moja kutoka eneo la Mambrui kaunti ya Kilifi kwa mwezi wa sita sasa wanamtafuta jamaa yao aliyetoweka kwa njia tata. Omar Abdulrahim aliyekuwa dereva wa lori alitoweka Agosti mwaka jana na juhudi za kumtafuta hazijafua dafu. Hata hivyo, familia hii inasema ilimudu tu kupata simu na leseni ya kuendesha gari kichakani.