Zaidi ya watu milioni 800 barani Afrika wakumbwa na uhaba wa chakula

  • | K24 Video
    191 views

    Zaidi ya watu milioni 800 barani Afrika wanakumbwa na uhaba wa chakula. Hii ina maana kuwa takribani asilimia 39 ya watu katika bara hili wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa chakula cha kutosha. mabadiliko ya tabia nchi, uharibifu wa ardhi na changamoto nyingine zinakithirisha taswira hiyo. Wiki hii, Kenya iliandaa kongamano lililofanyika katika makao makuu ya shirika la umoja wa mataoifa linaloshughulikia mazingira ,UNEP, jijini Nairobi, ambapo wanasayansi, watafiti na wadau katika sekta ya chakula kutoka pembe zote za dunia walikutana kuwasilisha suluhisho linaloongozwa na utafiti wa kisayansi katika kukabiliana na changamoto hiyo.