Ziwa Turkana limefurika na kusababisha hasara

  • | Citizen TV
    376 views

    Zaidi ya wakazi elfu tatu wanaoishi katika vijiji vitatu ufuoni mwa Ziwa Turkana wanahitaji msaada wa dharura baada ya kupoteza makao yao. Hii ni baada ya Ziwa Turkana kufurika na kuingia majumbani mwao. Shule nne za msingi na makanisa kadhaa pia yamefurika. Ziwa Turkana linafurika huku kiangazi kikali kikishuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya Turkana.