Zoezi la kuwaondoa wakaazi kuwapeleka eneo salama laendelea katika mji wa Arques

  • | VOA Swahili
    362 views
    Waokoaji wakiwaondoa baadhi ya wakazi wa miji iliyoko kaskazini mwa eneo la mkoa wa Pas de Calais Jumatano (Januari 3) wakati maji ya mafuriko yalipojaa mitaani na majumbani baada ya siku kadhaa za mvua kubwa zilizo sababisha mito kadhaa kufurika. Anthony Richevin na familia yake walikuwa kati ya wakaazi kadhaa walioondolewa kutoka mji wa Arques. Alisema nyumba zao zilizama sentimita 50 ndani ya mafuriko, na kuzifanya zisiweze kukaliwa kwa wakati huu. “Mara ya kwanza (mafuriko yalipotokea), nilidhania ilikuwa tu bahati mbaya. Lakini hivi sasa, kutokea hili mara ya pili, inaanza kutupa maumivu, iwe kwa hali ya kuwa na morali au hali ya bajeti yetu. Tunajiuliza vipi tutaweza kuvuka hili,” alisema Richevin. Hili ni tukio la pili la mafuriko katika mkoa wa Pas-de-Calais katika kipindi cha miezi mitatu. Mwezi Novemba, wakazi wengi wa Arques walishuhudia wiki tatu za mafuriko yaliyoharibu nyumba zao na mashamba yao. Kwa mujibu wa Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya Ufaransa mkoa huo utaendelea kushuhudia mvua zinazo nyesha mfululizo mpaka siku ya Ijumaa (January 5). - Reuters #mafuriko #Uingereza #dhoruba #henk #mvua #upepo #southernengland #wales #voa #voaswahili #ufaransa #mkoa #pasdecalais #arques #wakaazi