Mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei amesema akiba ya wananchi na pesa za malipo ya uzeeni hivi karibuni zitafadhili taifa hili katika kutekeleza miradi ya miundo-mbinu kama vile barabara, mabwawa na uunganishaji umeme kupitia mpango wa ushirikiano kati ya serikali na sekta ya umma. Akiongea wakati wa mkutano wa kila mwaka wa mpango pensheni wa kampuni TelPosta, Koske alisema wale wanaochangia kwenye mpango wa pensheni wamefanikiwa kuweka akiba ya shilingi trilioni 2.9 . Koskei alielezea umuhimu wa kuwepo kwa mpango wa uwekezaji sawa ili kurahisisha kutegemewa kwa mali na kuleta uthabiti wa muda mrefu.Mkuu huyo wa utumishi wa umma alisema ni muhimu kuhakikisha wale wanaostaafu wanapata malipo yao haraka iwezekanavyo na kutaka usimamizi bora.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive