- 9,125 viewsDuration: 2:40Gavana wa zamani wa Kiambu ferdinand Waititu amepata pigo kubwa baada ya Mahakama Kuu kuamuru kutwaliwa kwa mali yake ya thamani ya Shilingi milioni 76.2. Aidha mahakama pia imeamrisha kuwa sehemu ya ardhi ya Shilingi milioni 3 inayomilikiwa na mkewe Susan Wangari Ndūng'ū irejeshwe. Hii ni kufuatia kesi iliyowasilishwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) ikidai kuwa Waititu alijipatia mali ya shilingi bilioni 1.94 kwa njia tatanishi alipokuwa mbunge wa Kabete na baadaye akiwa gavana wa Kiambu.