Serikali imepongeza maafisa wa polisi wa Kenya waliohudumu katika taifa la Karibiani lililokumbwa na ghasia la Haiti chini ya ujumbe wa kimataifa wa kudumisha usalama, ikisema kwamba walitekeleza wajibu wao vyema licha ya ukosoaji wa mapema na taarifa potovu zilizoenea kuhusu kutumwa kwao. Maafisa hao, ambao wamerejea baada ya kukamilisha muda wao wa kuhudumu nchini humo, walikuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Wakenya kilichotumwa Haiti mwezi Juni mwaka 2024.Waziri wa usalama wa taifa Kipchumba Murkomen, aliyekutana na maafisa hao na kupata staftahi pamoja katika chuo cha mafunzo ya polisi wa utawala eneo la Embakasi, aliwasifu kwa kudumisha nidhamu, weledi, na kuheshimu viwango vya haki za binadamu walipokuwa wakitekeleza majukumu yao katika mazingira magumu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive