LISHE BORA
Wataalam wa lishe nchini Kenya wametoa wito kwa serikali ijumuishe huduma za lishe kwenye hazina ya bima ya afya ya jamii (SHIF). Akizungumza wakati wa kufungwa kwa kongamano la 5 la kimataifa kuhusu lishe lililoandaliwa Mlolongo, Kaunti ya Machakos, Afisa mkuu mtendaji wa taasisi ya masuala ya lishe Dkt. David Okeyo, alisema hatua hiyo itasaidia kushughulikia kikamilifu magonjwa yanayowakumba Wakenya. Aidha, alisema kuhusisha wataalam wa lishe katika utekelezaji wa mpango wa afya kwa wote kutasaidia kupunguza utapiamlo miongoni mwa watoto na kupunguza gharama ya kutibu madhara yake.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive