- 27,046 viewsDuration: 6:54Barabara kuu ya Rironi kuelekea Mau Summit, ni mojawapo ya miradi kuu ya serikali iliyozinduliwa na Rais William Ruto mwishoni mwa Novemba. Barabara hiyo inatarajiwa kubadilisha barabara ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikishuhudia msongamano mkubwa wa magari na ajali nyingi, ikiunganisha Nairobi na maeneo ya Bonde la Ufa na Magharibi mwa Kenya, pamoja na Afrika Mashariki.