- 11,791 viewsDuration: 1:23Onfon Mobile, kampuni inayouza simu kwa mkopo, imesisitiza tena dhamira yake ya kutoa huduma bora kwa wateja wake baada ya tukio ambapo baadhi ya wateja walishindwa kufungua simu zao licha ya kuendelea kulipa mikopo yao. Meneja Mkuu wa Onfon mobile Dennis Kuria, ameeleza kuwa tatizo hilo lilitokana na changamoto za kimfumo, ambazo kwa sasa zimeshatatuliwa.