Serikali inanuia kununua ardhi na kujenga taasisi ya kisasa ya Shule ya Filamu, ambayo itakuwa na ukumbi na studio za kisasa zenye vifaa vya kidijitali. Waziri wa Masuala ya Vijana, Uchumi wa Ubunifu na Michezo, Salim Mvurya, amesema kuwa taasisi hiyo pia itakuwa na afisi za wahadhiri na jukwaa ambalo litatumika kuwakuza vijana wanaotaka kubobea katika tasnia ya filamu na sanaa. Mvurya, aliyeongoza sherehe za nne za kuhitimu za shule hiyo katika uwanja wa Michezo wa Kasarani, alisema kuwa sekta ya filamu humu nchini inaendelea kukua, akiwahimiza vijana kuchukua fursa hiyo. Wahitimu 94 waliofuzu wamepewa changamoto za kutumia ujuzi wao kutafuta fursa za ajira katika soko la filamu inaloendelea kukua.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive