Watu wanane miongoni mwao watoto wawili walio chini ya umri wa miaka miwili wamefariki kufuatia ajali mbaya ya barabarani katika eneo la Bw’arani–Tombe kati ya Ekerenyo na mji wa Ikonge, kwenye barabara kuu ya Kisii-Kericho kaunti ya Nyamira. Ajali hiyo ambayo ilitokea jana mwendo wa saa mbili usiku, baina ya trela na gari la abiria lililokuwa likitoka jijini Nairobi, iliacha familia kadhaa zikiomboleza na watu wengine wakiuguza majeraha hospitalini. Gavana wa Nyamira Amos Nyaribo amesema serikali yake imebuni kamati maalum kufanikisha usaidizi wa haraka kwa manusura na familia za wale waliopoteza wapendwa wao.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive