Wakazi zaidi ya 5,000 wa kijiji cha Kavunyalalo, katika kaunti ndogo ya Malindi, kaunti ya Kilifi wamenufaika na mradi wa maji unaonuiwa kuboresha maisha yao. Mradi huo umefanikishwa na ushirikiano kati ya kampuni ya Danco Plastics na shirika la AMREF.
Wakazi hao pia walipokea mabomba na vifaa vya kuunganisha maji kutoka kisima hicho hadi nyumbani na mashambani mwao. Wanasema mradi huo utawasaidia sio tu kupata maji ya kutumia nyumbani mbali pia ya kuendeleza shughuli za kilimo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive