Kampeni ya chanjo inayowalenga maelfu ya watoto katika kaunti ya Migori na maeneo yaliyo karibu inatarajiwa kuanza mwezi ujao kama sehemu ya juhudi mpya ya wadau katika sekta ya afya kutokomeza ugonjwa wa Polio nchini. Akizungumza wakati wa matembezi ya kukabiliana na ugonjwa huo, msimamizi wa kilabu cha Rotary eneo la 9212, Wairimu Njage alisema mpango huo unanuiwa kuhakikisha watoto kwenye maeneo yanayokabiliwa na hatari kubwa ya maambukizi wamekingwa dhidi ya ugonjwa huu wa kupooza.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive