Watu saba wamethibitishwa kufariki katika matukio mawili tofauti ya ajali za barabarani. Sita walifariki kwenye barabara kuu ya Nakuru-Gilgil kufuatia ajali ya kugongana dafrao baina ya gari dogo aina ya Saloon na basi eneo la Soysambu. Akithibitisha tukio hilo, msimamizi wa kituo cha polisi cha Gilgil Winston Mwakio alisema waathiriwa walikuwa wakisafiria katika gari dogo aina ya Saloon wakati lilipogongana na basi mwendo wa saa kumi alfajiri siku ya Jumamosi. Na huko Kamundura, dereva wa lori alipoteza mwelekeo wakati lori hilo lilipokosa breki. Ripoti zinaonesha kwamba lori hilo liligonga duka la kuuzia vifaa vya ujenzi na kumuua mwenyewe papo hapo. Timothy Kipnusu na habari kwa kina.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive