Raia sita wa Iran wanaohusishwa na shehena ya dawa za kulevya aina ya methamphetamine ya thamani ya shilingi bilioni 8.2 iliyonaswa katika kaunti ya Mombasa watajua hatma yao hapo kesho katika mahakama ya Shanzu. Wapelelezi na idara ya mashtaka ya umma hivi leo waliomba siku 14 kukamilisha uchunguzi, wakidai kikwazo cha lugha. Sita hao walikamatwa Ijumaa iliyopita kufuatia operesheni ya mashirika mbalimbali ambapo mifuko 769 inayoaminika kuwa ya dawa za kulevya aina ya methamphetamine, yenye uzani wa tani moja ilipatikana.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News