- 8,771 viewsDuration: 3:25Rais William Ruto anasema serikali itanunua vifaa vinavyohitajika kusaidia jeshi la taifa kufungua kambi za kiusalama katika kaunti zinazokabiliwa na utovu wa usalama. Ruto amesema kambi hizo ni sehemu ya juhudi pana za serikali za kuimarisha uwezo wa Kenya wa kukabiliana na vitisho vya kiusalama vua ndani na nje ya nchi. Alitoa wito kwa wale watumishi wa umma, ikiwa ni pamoja na wanajeshi, kutokomeza utepetevu kazini ili kuboresha huduma kwa wananchi. Rais alisema haya wakati wa maadhimisho ya siku ya jeshi ya mwaka huu katika kambi ya wanajeshi ya Moi mjini Eldoret, kaunti ya Uasin Gishu. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive