- 1,945 viewsDuration: 3:21Mipango ya awali ya kuweka mwili wa marehemu Raila Odinga katika majengo ya Bunge kwa ajili ya kuuagwa na umma ilisitishwa, baada ya umati wa waombolezaji waliokuwa wamekusanyika hapo kuzua vurugu, hali iliyolazimu shughuli hiyo kuhamishiwa katika uwanja wa Kasarani. Waombolezaji waliokuwa wamefika kuaga mwili wa Raila waliwazidi polisi nguvu na kuvunja vizuizi vya usalama Bungeni. Hali ya taharuki iliongezeka huku baadhi ya waombolezaji wakijaribu kuingia ndani ya majengo ya Bunge, jambo lililowalazimu wabunge kuingilia kati na kuwataka waombolezaji watulie na kudumisha utulivu na heshima. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive