Tume ya maadili na kupambana na ufisadi hapa nchini imerejesha ardhi ya ekari 7.11 ya thamani ya shilingi Bilioni 2.8 ambayo ilikuwa imenyakuliwa katika msitu wa Karura, na taasisi ya mafunzo ya kiufundi. Katika uamuzi wake mnamo Oktoba 23 mwaka huu, mahakama ya kushughulikia kesi za mazingira na ardhi ilifutilia mbali hati miliki ya ardhi hiyo ya kampuni ya Gigiri Court ambayo ilinunua ardhi hiyo kutoka kwa aliyekuwa waziri wa mazingira Marehemu John Joseph Kamotho, anayesemekana kupata vipande hivyo viwili vya ardhi kwa njia haramu. 
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
 
#kbcchannel1 #news  #kbclive