Rais William Ruto amejitetea kwa kutia saini mswada wa matumizi mabaya ya tarakilishi na uhalifu wa mtandaoni pamoja na miswada mingine saba kuwa sheria. Rais alisema sheria hiyo, ambayo utekelezaji wake umesitishwa kwa muda na Mahakama Kuu, unalenga kulinda watu dhidi ya unyanyasaji mtandaoni, itikadi kali za kidini na ugaidi. Alikuwa akihutubia waombolezaji kwenye mazishi ya babake Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja, Mzee Weston Kirocho Kanja, katika kaunti ya Laikipia.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive