- 27,988 viewsDuration: 3:29Rais William Ruto amewaonya baadhi ya Wakenya anaosema wanaeneza uongo na uvumi kuhusu sheria mpya ya kudhibiti utumizi wa mitandao. Rais akisema sheria hiyo inalenga kuzuia ugaidi, mahubiri potovu na mitandao ya ngono nchini. Akizungumza kaunti ya Laikipia, Rais Ruto aidha alikanusha madai kwamba alitia saini mswada huo, licha ya taifa kuwa kwenye maombolezo ya aliyekuwa waziri mkuu, hayati Raila Odinga.