Rais William Ruto amesema kenya itapanda ngazi kutoka taifa linalostawi hadi taifa lililostawi katika muda wa miaka 30 ijayo. Akiongea wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya kanisa la African Inland, Ziwani yaliyoandaliwa katika shule ya Starehe Boys, kaunti ya Nairobi, Ruto alisema serikali yake imeweka msingi wa kuafikia hatua hii katika mwaka wa 2055. Wakati uo huo, alisema amebadilishana maono na rais mstaafu Uhuru Kenyatta, kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga na mwenyekiti wa chama cha KANU Gideon Moi ambaye hivi majuzi alijiunga na serikali jumuishi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive