Wakazi wa Kijiji cha Dhololo katika wadi ya Magarini, Kaunti ya Kilifi, wanakabilwa na uhaba mkubwa wa maji huku ukame ukiendelea kukumba eneo hilo. Wenyeji wanasema hali hiyo inawalazimu kuamka kabla ya mawio ya jua na kutembea takriban kilomita kumi na mbili kuchota maji kutoka kisima kilicho eneo jirani la Kambicha. Hali hii pia imeathiri wanafunzi, kwani shule nyingi hazina maji jambo ambalo linahatarisha afya yao.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive