Wakazi wa kijiji cha Mwembetsungu kilichoko eneo bunge la Kilifi Kusini, Kaunti ya Kilifi, waliandamana wakidai kufidiwa kwa ardhi yao iliyotwaliwa na kampuni ya kusambaza umeme, KETRACO. Wakazi hao wanadai kwamba kampuni ya KETRACO ilianzisha mradi wa umeme unaopitia kwenye ardhi yao, hatua iliyosababisha sehemu za mashamba kutumika kwa utekelezaji wa mradi huo, huku kampuni hiyo ikiahidi kuwalipa fidia baada ya miezi mitatu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive