Skip to main content
Skip to main content

Watu 7 wafariki katika ajali tofauti za barabarani nchini

  • | KBC Video
    328 views
    Duration: 2:11
    Watu saba wamethibitishwa kufariki katika matukio mawili tofauti ya ajali za barabarani. Sita walifariki kwenye barabara kuu ya Nakuru-Gilgil kufuatia ajali ya kugongana dafrao baina ya gari dogo aina ya Saloon na basi eneo la Soysambu. Akithibitisha tukio hilo, msimamizi wa kituo cha polisi cha Gilgil Winston Mwakio alisema waathiriwa walikuwa wakisafiria katika gari dogo aina ya Saloon wakati lilipogongana na basi mwendo wa saa kumi alfajiri siku ya Jumamosi. Na huko Kamundura, dereva wa lori alipoteza mwelekeo wakati lori hilo lilipokosa breki. Ripoti zinaonesha kwamba lori hilo liligonga duka la kuuzia vifaa vya ujenzi na kumuua mwenyewe papo hapo. Timothy Kipnusu na habari kwa kina. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive