Utekaji Nyara | Waziri Blinken ataka uwajibikaji wa vyombo vya usalama

  • | Citizen TV
    2,196 views

    Marekani imejiunga na mataifa mengine ya kigeni katika kushinikiza uwajibikaji kutoka kwa vyombo vya usalama vya Kenya kuhusu matukio ya kutoweka na utekaji nyara wakati wa maandamano ya Juni hadi Agosti. Katika mazungumzo na Rais William Ruto Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken, pia alisisitiza umuhimu wa kuendelea na mazungumzo na wananchi, mashirika yasiyo ya serikali na vijana.