Serikali kwa ushirikiano na TBK, inalenga kuimarisha uuzaji na uboreshaji wa majani

  • | K24 Video
    20 views

    Serikali kwa ushirikiano na bodi ya usimamizi wa majani chai nchini, TBK, inalenga kuimarisha uuzaji na uboreshaji wa majani chai ili kuongeza pato la kigeni pamoja na kuimarisha mafao ya wakulima laki nane wanaoendeleza kilimo hicho. Kulingana na katibu katika wizara ya kilimo na mifugo daktari Paul Runo kuondolewa kwa ushuru unaoathiri sekta hiyo na kuimarishwa kwa soko la kimataifa kutaongeza pato la kitaifa linalochangiwa na sekta hiyo kutoka asilimia 2 hadi 10.