Russia iliionya Marekani kabla ya kufyatua kombora la Oreshnik
Msemaji wa Kremlin amesema leo Ijumaa kwamba Moscow iliipelekea Marekani onyo dakika 30 kabla ya kufyatua kombora jipya la masafa ya kati huko Ukraine.
Kremlin iliruhusu kufyatuliwa kombora hilo jipya lililopewa jina la Oreshnik dhidi ya mji ulio kati kati mwa Ukraine wa Dnipro jana alhamisi.
Rais Putin amesema kwenye hotuba yake kwamba shambulio hilo limefanyika kujibu hatua ya Kyiv wiki hii kutumia makombora ya Marekani na Uingereza yenye uwezo wa kufika mbali ndani ya Russia.
Putin alionya kwamba mfumo wa Marekani wa ulinzi wa anga hautaweza kuzuia kombora jipya ambalo anasema lina safiri kwa kasi ya mara 10 zaidi ya sauti.
Hii leo pia msemaji Peskov aliulaumu utawala wa hivi sasa wa Marekani kwa kuzorotesha ugomvi wa Ukraine na kusema kwamba hakuna mawasiliano kati ya Moscow na Washington juu ya suala hili. - AP
Wakati huo huo Waziri wa ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov amesema serikali yake ilikuwa inaongeza uwezo wa ulinzi wa anga wakati ikijibu mashambulizi ya makombora ya masafa marefu ya Russia katika mji wa ukarine wa Dnipro.
Umerov ameyasema hayo leo katika maelezo yake kwa vyombo vya habari akiwa na mwenzake wa Sweden Pal Johnson mjini Stockholm.
Jonson ameongeza kuwa shambulizi la Russia haliwezi kuikatisha tamaa uungaji mkono wa serikali yake kwa Ukraine.
Alhamisi Russia ilifyatua makombora ya masafa marefu kujibu hatua ya Marekani na Uingereza kuiruhusu Kyiv kushambulia ndani ya ardhi ya Russia na silaha zake za Magharibi za ubora wa juu.
- AP and Reuters
#voaswahili #afrika #ukraine #russia #kombora #oreshnik #dnipro #moscow #russia
23 Nov 2024
- The move comes just a day after Governor Anne Waiguru's sentiments.
23 Nov 2024
- The incident happened three months ago and left the constable's wife nursing gunshot injuries.
23 Nov 2024
- The announcement follows a week after Meg Whitman tendered her resignation.
23 Nov 2024
- President-elect Donald Trump said he will nominate hedge fund manager Scott Bessent as secretary of the Treasury, in a statement Friday night.
23 Nov 2024
- Taboos and misinformation are fueling period stigma and poverty in the country, amid calls to promote menstrual health and dignity. Menarche, which is the onset of menstruation, varies from person to person, typically occurring between the ages of 10…
23 Nov 2024
- Detectives from the Directorate of Criminal Investigations (DCI) have arrested a 27-year-old man in connection with the fatal shooting of another man in Eastleigh's California Estate on November 9.
23 Nov 2024
- The number of Kenyans seeking loans from digital lenders has been on the rise in the last two years due to the harsh economic times.
23 Nov 2024
- The runner-up in Mozambique's October 9 presidential elections, Venancio Mondlane, has accepted President Filipe Nyusi's offer to join discussions with him and three other candidates in hopes of ending weeks of postelection protests and violence that…
23 Nov 2024
- The move comes just a day after Governor Anne Waiguru's sentiments.
23 Nov 2024
- Why is everything around President Ruto falling apart?
23 Nov 2024
- EACC nominates Abdi Mohamud as new CEO to replace Twalib Mbarak
23 Nov 2024
- A listening president? Ruto's new statements signal change of tack
23 Nov 2024
- Lawyer battles with client over Sh17.5m from property sale