Upinzani wakamatwa, wazuiliwa kuwasilisha malalamiko ubalozi wa Kenya

  • | VOA Swahili
    30 views
    Viongozi wa kisiasa wa Uganda wamekamatwa baada ya kufanya maandamano wakielekea Ubalozi wa Kenya, mjini Kampala. Viongozi hao walikuwa wanataka kuwasilisha malalamiko yao katika Ubalozi wa Kenya wakitaka majibu juu ya kukamatwa kwa aliyewahi kuwa mgombea urais Dr Kizza Besigye, ambaye pia ni mpinzani mkuu wa kisiasa wa Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni, katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Novemba 16, 2024. - Ripoti ya mwandishi wa VOA Saddam Muballe, Kampala, Uganda #voaswahili #afrika #uganda #besigye #museveni #upinzani ⁣