Mawakili wa Kenya wazuiliwa kumuwakilisha Kizza Besigye mahakamani Uganda

  • | Citizen TV
    2,472 views

    Kinara wa Narc Kenya Martha Karua na mawakili wengine kutoka Kenya walifika mbele ya mahakama ya kijeshi nchini Uganda walizuiliwa kumwakilisha kiongozi wa upinzani wa nchi hiyo Dkt. Kizza Besigye. Karua alifahamishwa kuwa hangeweza kumwakilisha Besigye kwa kuwa hana cheti cha kumpa ruhusa nchini Uganda. Kulingana na mkewe Besigye Winnie Byanyima, maafisa wa Uganda waliwazuia zaidi ya mawakili ishirini kutoka kenya dhidi ya kumtetea mumewe ambaye alitekwa nyara humu nchini na kufikishwa nchini uganda alikozuia. Besigye anakabiliwa na mashtaka ya kumiliki silaha pamoja na tisho kwa usalama.