Biden akagua gwaride, aungana na Rais wa Angola kusalimiana na viongozi

  • | VOA Swahili
    613 views
    Rais wa Marekani Joe Biden leo amekagua gwaride lililotayarishwa kwa heshima yake katika mji wa Luanda. Baada ya zoezi hilo la kukagua gwaride akiwa na mwenyeji wake Rais wa Angola Rais wa Angola Joao Lourenco, alisalimiana na maafisa wa serikali ya Angola na pia maafisa wa ubalozi wa Marekani nchini humo. Biden aliwasili Angola Jumatatu kuanza ziara yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu huko Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara na atatumia siku tatu za ziara yake kukabiliana na ushawishi wa China kwa kutangaza mradi wenye matarajio makubwa wa reli unaofadhiliwa na Marekani. Ujenzi wa reli unaojulikana kama Lobito Corridor unaofufuliwa tena huko Zambia, Congo na Angola una azma ya kuendeleza uwepo wa Marekani katika eneo lenye utajiri wa madini muhimu yanayotumiwa kutengeneza betri za magari ya umeme, vifaa vya kieletroniki na teknolojia ya nishati safi. ⁣ #biden #us #angola #luanda #voa