NCCK inaonya taifa lipo katika hali mahututi

  • | Citizen TV
    622 views

    Baraza la makanisa nchini (NCCK) sasa linaonya kuwa taifa lipo katika hali mahututi. Wakizungumza baada ya mkutano wa baraza kuu, viongozi hao wa makanisa wamemtaja rais william ruto kuwa mwongo na mwenye kuhujumu haki za kibinaadam. NCCK imewakashifu wabunge na maseneta na kusema kwua wamekuwa vibaraka wa serikali badala ya kuwatetea waliowachagua, na kuwataka wananchi kuanza mchakato wakuwaondoa ofisini.