Gavana wa Kaunti ya Kilifi anawaweka maafisa wabadhirifu katika tahadhari.

  • | KBC Video
    88 views

    Kitengo maalum kimebuniwa kukomesha wizi wa dawa katika kaunti ya Kilifi.Hatua hii inafuatia kukamatwa kwa maafisa wawili wa serikali ya kaunti ya kilifi kwa madai ya wizi wa dawa za thamani ya shilingi elf-100 kutoka hospitali moja eneobunge la Ganze siku mbili zilizopita. Gavana wa kaunti ya kilifi, Gideon Mung`aro ambaye alikuwa akizundua mradi wa kukarabati barabara ya Mtondia na madarasa ya kisasa katika shule ya Chekechea ya Tezo alisema kitengo hicho kitajumuisha wananchi na maafisa wa kaunti huku akiwahimiza wakazi kutoa taarifa ambazo zitawezesha kukamatwa kwa washukiwa zaidi wa wizi wa dawa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive