Bwawa la Miaani lavunja kingo na kuharibika kabisa

  • | Citizen TV
    961 views

    Seneta wa Makueni Daniel kitonga Maanzo ameitaka serikali ya Makueni kumfanyia uchunguzi muandisi anayesimamia ujenzi wa mabwawa katika kaunti hiyo na kumchukulia hatua kufuatia kuvunjwa kwa ukuta wa bwawa la Miaani lililoko katika eneo la Kibwezi mashariki. Bwawa hilo liliharibiwa na maji hata kabla ya kumalizika kujengwa, wakazi wakiwa kwenye hatari ya kupoteza shilingi milioni kumi kwenye ujenzi wa bwawa hilo.