Juhudi za kusafisha Los Angeles, operesheni ya uokoaji zaendelea

  • | VOA Swahili
    88 views
    Wiki moja baada ya moto mkubwa kuzuka California na kusambaa bila kudhibitiwa, watabiri wa hali ya hewa wanabashiri kwamba upepo mkali na hatari unaojulikana kama santa Ana unaweza kutokea. Baadhi ya maeneo ya Los Angeles na mengine Jirani ya jimbo la Ventura yako katika hali ya hatari . Hata hivyo maafisa wamesema wako tayari kwa ajili ya vitisho vyovyote kutokana na moto huo, hasa katika maeneo ambayo tayari yameungua moto na ni makavu . Gavana wa California Gavin Newsom Jumanne aliamuru timu za kuondoa vifusi kuwa tayari huku wasimamizi wa dharura wakitarajia Dhoruba za msimu wa baridi ambazo zinaweza kusababisha maporomoko ya matope. Baadhi ya wakaazi wa Palisades wameamua kutosubiri wakifanya kazi ya kuondoa uchafu ulioungua barabarani. #marekani #la #wildfires #voaswahili #santamonica #malibu #makazi #california #losangeles