Waislamu wasiosali wala kufunga Senegal

  • | BBC Swahili
    22,715 views
    Hawasali, hawafungi, wanafuga nyewele zao kwa mashungi au rasta na kuvalia nguo zenye rangi nyingi na viraka…Hapa nawazungumzia Baye Fall, kikundi cha Waislamu nchini Senegal kinachoibua maswali kutoka kwa makundi ya kihafidhina ya kiislamu ndani na nje ya nchi hiyo kwa namna imani yao ilivyo tofauti na Uislamu uliozoeleka. Nguzo kuu za imani yao ni kujitolea kufanya kazi kwa bidii na kwa nguvu zote na dhana ya 'Ndiguel', ambayo ni kujitolea kumtumikia sheikh au Khalifa wao. Taarifa hiii ya mshindi wa tuzo ya BBC ya Komla Dumor Rukia Bulle inawasilishwa na Agnes Penda. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw