Familia za Mlolongo 3 zaendelea kuomba haki zikiashiria kuchoshwa na taasisi za serikali

  • | K24 Video
    13 views

    Familia za Mlolongo 3. Justus Mutumwa, Martin Mwau, na Karani Muema zinaendelea kuomba haki, zikiashiria kuchoshwa na taasisi za serikali huku zikisaka majibu kuhusu waliko wapendwa wao. Mapema leo, familia za waathiriwa hao zilizuiliwa kuingia mahakamani, maafisa wa usalama wakisema walikuwa na maagizo kutoka kwa mamlaka ya juu. Hii inafuatia hatua ya inspekta jenerali wa polisi Douglas Kanja na mkuu wa DCI Mohammed Amin kususia kufika mahakamani. Badala yake, walifungua ombi la dharura wakitaka kuondoa maagizo ya mahakama yanayowataka kufika binafsi kutoa maelezo kuhusu kupotea kwa watatu hao waliotekwa nyara mlolongo.