Ruto : Machifu watano waliotekwa nyara lazima watapatikana

  • | KBC Video
    2,785 views

    Rais William Ruto amesema serikali yake itafanya kila juhudi kuhakikisha machifu watano waliotekwa nyara mnamo Jumatatu na washukiwa wa ugaidi wa Al Shabaab wamerejea salama. Rais Ruto aliyekuwa kwenye ziara katika kaunti ya Mandera alisema alikuwa ameziagiza asasi zote za usalama kuhakikisha viongozi hao wameachiliwa. Rais Ruto aliahidi vita dhidi ya makundi ya uhalifu akisema Mandera ni lazima ifaidi amani kama mji wowote mwingine nchini Kenya.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive