Wagonjwa wa saratani walalamikia ukosefu wa dawa

  • | KBC Video
    28 views

    Waathiriwa wa ugonjwa wa Saratani pamoja na mashirika ya kijamii yameiomba serikali kuhakikisha upatikanaji endelevu wa matibabu ya saratani katika hospitali zote za umma kufuatia madai ya kutopatikana kwa Herceptin, dawa muhimu inayotumiwa kutibu saratani ya titi. Wakihutubia wanahabari wakati maadhimisho ya siku ya kukabiliana na ugonjwa huo duniani katika jiji la Nairobi, Muungano wa mashirika ya kukabiliana na ugonjwa humu nchini pamoja na chama cha waathiriwa wa ugonjwa yaliihimiza serikali kuwianisha huduma za matibabu chini ya SHA ili kuhakikisha kuna huduma endelevu ya matibabu .

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive