Trump: Marekani inaweza 'kuichukua' Gaza

  • | BBC Swahili
    1,035 views
    Rais Donald Trump amesema kuwa watu wa Palestina wanaweza kuhamishwa katika mataifa mengine huku Marekani ikichukua Gaza ili kuondoa mabomu ambayo hayajalipuka, kujenga upya na kuendeleza upya eneo hilo kiuchumi. Alikuwa katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, ambaye alisema wazo la Trump "linafaa kupewa kipaumbele". Ukanda wa Gaza umezungukwa na Israel, Misri na Bahari ya Mediterania. Tarehe 7 Oktoba 2023, Hamas ilishambulia Israeli na kuua watu wapatao 1,200 na kuchukua zaidi ya mateka 250. Hii ilisababisha mashambulizi ya kijeshi ya Israel ambapo zaidi ya watu 47,400 wameuawa, kwa mujibu wa wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas. #bbcswahili #marekani #trump Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw