Familia moja Lungalunga yahangaika baada ya mwili wa mpendwa wao kukwama nchini Saudi Arabia

  • | Citizen TV
    758 views

    Familia moja katika kijiji cha Tswaka eneo la Lungalunga kaunti ya Kwale inahangaika baada ya mwili wa mpendwa wao kukwama nchini Saudi Arabia kwa zaidi ya wiki moja sasa. Familia hiyo inasema mpendwa wao Mwandazi Athuman Mohamed aliaga dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi na mwajiri wake anadai atauzika mwili wake huko iwapo itashindwa na kuusafirisha.