Tasnia ya habari nchini inaomboleza Mambo Mbotela

  • | Citizen TV
    2,285 views

    Jumbe za rambirambi zinaendelea kumiminika kwa mtangazaji maarufu Leonard Mambo Mbotela, ambaye alifariki Ijumaa asubuhi akiwa na umri wa miaka 85. Mbotela, amekumbukwa kama mtangazaji nguli katika tasnia ya habari nchini. Alikubalika kwa ustadi wake wa kujieleza, na uwezo wake wa kipekee wa kuunganisha vizazi.