Marais washinikiza mazungumzo ya amani mashariki mwa DR Congo

  • | Citizen TV
    1,907 views

    Rais William Ruto, ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amepuuzilia mbali utumizi wa majeshi kama suluhu ya mapigano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kwenye mkutano uliowaleta pamoja marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya mataifa ya kusini mwa afrika mjini Dar es salaam Tanzania, rais ruto amesema kuwa mazungumzo ndio njia ya pekee ya kusitisha mapigano na kurejesha amani. Mkutano huo ulimtaka rais wa Congo Felix Tshisekedi ambaye alihudhuria mkutano kwa njia ya mtandao, kufanya mazungumzo na waasi wa M23.